KUHUSU Kuvunja Ndoa ya Kiba, Mchekeshaji Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii wa vichekesho Bongo maarufu kwa jina la Martha, amefunguka juu ya kuwa chanzo cha kuiweka pabaya ndoa ya msanii Abdu Kiba, na kusema kwamba yeye hahusiki kwa lolote

Akizungumza kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Martha amesema kwamba licha ya kuwa aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Abdu Kiba, lakini kwa sasa hayuko naye tena, hivyo habari za kuwa chanzo cha migogoro ya ndoa yake sio kweli.

Akiendelea kufunguka juu ya mahusiano yake na Abdu Kiba, Martha amesema Abdu Kiba amekuwa akimtafuta mara kwa mara kwa njia ya simu, lakini hakuna chochote kinachoendelea kati yao, kwani sasa wamebaki marafiki wa kawaida.

“Nilikuwa natoka naye, mara nyingi ananicheck, toka nimetoka kwake tayari nilikuwa na mahusiano na mtu mwingine, ni mwanaume ambaye nilikuwa naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu,  lakini kuvunja ndoa  yake sijui, tangu ameoa sijamfuatilia lakini yeye ndio amekuwa akinifuatilia sana, mimi nachati naye tu, mimi sijui kama mkewe anachukia”, amesema Martha.

Sambamba na hilo Martha amekwenda mbali zaidi kwa kusema hata mke wake hapaswi kuchukia kwani anatakiwa atambue kabla yeye hajaolewa, kuna watu walikuwa kwenye mahusiano na mume wake.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad