Monalisa Agoma Kuitwa BIBI Awatolea Povu Wanaomuita Hivyo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Monalisa agoma kuitwa BIBI
Staa wa filamu nchini, Monalisa amewachamba wanaomuita 'Kibibi' baada ya kutokea kwenye video ya msanii wa Bongofleva Ben Pol, ambayo inakwenda kwa jina la Ntala Nawe.

Akizungumza na eNewz, Mona amesema kuwa hakushtushwa na 'comment' za mashabiki  wa Ben Pol ambao baada ya kuona video hiyo walianza kuhoji  kuwa kwa nini Ben Pol hajachukua wasichana wadogo na kumuweka yeye.

"Kila mtu ana mtazamo wake na kwangu mimi hicho ni kitu cha kawaida  watu lazima tu wataongea midomo wameumbiwa ili kuongea ila poleni sana na itabidi tu muiangalie video kwa sababu Ben Pol ndio mtu ambaye amenichagua na ameona ninapendeza kwenye video yake" alisema.

Monalisa aliongeza kuwa alikuwa tayari kufanya video hiyo bure bila malipo yoyote kwa kuwa anamkubali Ben Pol lakini msanii huyo alimpa kiasi fulani cha pesa na alimwambia thamani aliyonayo ni kubwa sana na anajua hatoweza kumlipa kiasi kinachoweza kufikia thamani hiyo.

Alimaliza kwa kusititiza kuwa 'hawezi kukataza mitazamo ya watu kwani si kila mtu atapenda utakachokifanya''.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad