Rapper Young Thug Aangusha Chozi Mahakamani , Aachiwa Huru

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rapper Young Thug aangusha chozi Mahakamani , aachiwa huru
Ifahamu hii kutokea Marekani ambapo Rapper Young Thug ameachiwa huru kutoka jela na hii ni baada  ya kesi yake kusikilizwa mapema leo November 15,2018 na ameiomba radhi Mahakama kwa makosa aliyoyatenda.

Rapper huyo alikamatwa wiki iliyopitwa mjini Georgia na kurudishwa jela ikiwa kosa lake ni kwenda kinyume na masharti ya dhamana  na kushindwa kuwasilisha vipimo vya afya wakati alipokuwa chini ya uangalizi (Probation).

Rapper Young Thug bado anakabiliwa na mashtaka mengine 8 ya jinai ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya pamoja na silaha mwezi September,2017, inaelezwa kuwa rapper huyo anahitajika kuhudhuria ushauri na saa juu ya matumizi ya dawa za kulevya  na kuwasilisha vipimo vya dawa za kulevya Mahakamani kila baada ya wiki mbili.

“Samahani kwa kutoitii Mahakama , samahani kwa kutomtii Muendesha Mashataka na kuwepo hapa kwa mara nyingine tena, nataka kwenda nyumbani nikaonane na familia yangu na kufanya vitu vilivyosahihi”

Rapper Young Thug amejutia makosa yake mbele ya Mahakama  na wakili wake kusema kuwa tayari amejiadhibu mwenyewe kwa kutokula chakula kwa siku mbili tokea ameingia jela wiki iliyopita.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad