Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kufanya Ziara Ya Siku Moja Nachingwea

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kufanya Ziara Ya Siku Moja Nachingwea
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa, anatarajiwa kutembelea Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Jumamosi ya tarehe 17, November 2018 .

Taarifa iliyotolewa hii leo Novemba 15, na Mbunge wa Nachingwea, Mhe. Hassani Masala inasema  kuwa, Mhe. Waziri mkuu atatua uwanja wa ndege wilayani Nachingwea mnamo saa mbili asubuhi akitokea Dodoma na kupokelewa na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Rukia Muwango pamoja na viongozi wengine wa serikali, kisha Waziri atafanya ziara ya siku moja katika wilaya hiyo kwa kutembelea tarafa ya kilimarondo.

"Mhe. Waziri Mkuu akiwa njiani kuelekea kilimarondo atasalimia wananchi wa Mtua na Mbondo kisha Mkutano wa hadhara mkubwa utakaobeba ujumbe wa wilaya utafanyika Kilimarondo na kujumuisha wananchi wote wa Kilimarondo,Matekwe na kiegei,  lakini Pamoja na kusalimia Wananchi na kusikiliza kero zao, Mh Waziri Mkuu atakagua na kujionea Ujenzi wa kituo cha Afya Kilimarondo"  Amesema Mhe. Masala.

Mbunge Masala amewaasa Wananchi wa Nachingwea tujitokeza kwa wingi saa moja asubuhi uwanja wa ndege tayari kwa kupokea ugeni huu aliosisitiza kuwa ni ugeni wa heshima kwao kama wilaya.

Nachingwea ni wilaya inayoongoza kwa kuzalisha Korosho nyingi mkoani Lindi kwa Msimu uliopita na hata huu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad