Mbunge: Nilitakiwa Kukeketwa na Kuolewa Nikiwa Darasa la nne

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Catherine Ruge amedai yeye ni miongoni mwa waathirika wa mila potofu ya ukekeketaji baada ya kutishiwa kutengewa na jamii iliyokuwa ikimzunguka kufuatia hatua yake ya kupinga waziwazi vitendo hivyo. 

Kwa mujibu wa Mbunge Ruge, mara baada ya kukataa kufanyiwa kitendo hicho, wazee wa kimila walimtishia kuwa asingeweza kuzaa kwa sababu alikiuka mila ambazo ziliasisiwa tangu enzi za kale. 

Akizungumza wilayani Serengeti, Catherine Ruge amesema ameamua kufanya hivyo kwa lengo la kumuokoa mtoto wa kike. 

“Nilitakiwa kukeketwa na kuolewa nikiwa darasa la nne na baada ya kukataa, nililaaniwa na kuambiwa sitafaulu mitihani, kuolewa wala kuzaa lakini nilisimama na Mungu na hatimaye nimefikia hapa nilipo,” amesema Catherine. 

“Baada ya kufaulu masomo hadi chuo kikuu, niliolewa, lakini nilikaa muda mrefu bila kuzaa hivyo wengine wakaamini ni laana,” alisema. 

“Ila mimi niliamini Mungu yupo na atanisaidia, muda tu ulikuwa haujafika. Sasa ni mama wa watoto wawili.” 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad