Mrembo wa Uganda ang’ara Miss World, afuata nyayo za Mtanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Hatimaye mshindi wa mashindano ya kumsaka Mrimbwende wa Dunia, Miss World 2018 ametangazwa leo kuwa ni mrembo kutoka Mexico, Vanessa Ponce, lakini Afrika imebebwa na mrembo wa Uganda, Quiin Abenakyo aliyetinga tano bora.


Abenakyo, ameibuka kuwa mshindi wa taji la Miss World Africa, akishika nafasi tano za juu zaidi katika mashindano hayo ya 68, hatua mbayo haijawahi kufikiwa na mwakilishi wa Uganda tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 1951.

Abenakyo amefuata nyayo za mrembo wa Tanzania, Nancy Sumari aliyenyakua taji hilo la Malkia wa Afrika (Miss World Africa) mwaka 2005. Kama ilivyo kwa Abenakyo, Nancy alikuwa Mtanzania wa kwanza kufika hatua hiyo tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo

Mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya mwaka huu, Queen Elizabeth Makune pia amefanya vizuri akiingia kwenye kinyang’anyiro cha warimbwende 100 waliokuwa na nafasi ya kutwaa taji la dunia. Hata hivyo, bahati haikuwa kwake, licha ya kuonekana kukubalika na wengi kupitia kura alizokuwa amepigiwa kura hizo hazikutosha kwenye mchakato huo pamoja na vigezo

Mexico imeandika historia ya kuchukua taji la Miss World kwa mara ya kwanza, huku nafasi ya pili ikienda kwa mrembo wa Thailand, Nicolene Limsnukan. Nafasi tatu za kukamilisha nafasi tano za juu zilienda kwa Uganda, Jamaica na Belarus.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad