RC Mgwira akerwa wanaoingia mitini na pesa za mkopo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, amesema tabia ya baadhi ya wanachama wa vyama vya akiba na mikopo kuchukua mikopo kisha kuhama vituo vya kazi kimya kimya ama kustaafu bila kutoa taarifa ni sawa na wizi na haikubaliki. 

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimali Watu katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo, Bwai Biseko, kwenye ufunguzi wa mkutano wa 21 wa chama cha akiba na mikopo cha walimu wa Moshi vijijini, Mghwira alitaka wanachama kuwa waadilifu. 

Akifungua mkutano huo, Dk. Mghwira alitaka wanachama kuhakikisha wanarejesha mikopo yao kwa wakati, ili fedha hizo zisaidie wanachama wengine wenye uhitaji. 

“Kitendo cha wewe mwanachama kupewa fedha, kisha kutozirejesha ama kuhama kituo cha kazi au kustaafu kimya kimya bila kuwaeleza viongozi wako, hiyo ni dhamira ya wizi na kimsingi ni utovu wa nidhamu kwa watumishi wa umma, tuikemee tabia hiyo,” alisema. 

Aidha, mkuu wa mkoa aliipongeza kada ya ualimu kwa kujijengea nidhamu na heshima ndani ya jamii na kuwataka kuepuka kuwa watumwe wa asasi za kifedha zenye masharti magumu ya mikopo ambayo huwatesa wanachama na kuwavunjia heshima. 

Mapema Mwenyekiti wa Sacco's hiyo, Christina Lyamuya, alisema chama hicho kimeingiwa na hofu ya kupata hasara ya zaidi ya Sh. milioni 83.5, baada ya wanachama wake ambao walikuwa walimu kufukuzwa kazi kutokana na kukutwa na vyeti feki na wasiyo na vyeti vya kidato cha nne. 

Alisema awali mikopo sugu ilikuwa na thamani ya Sh. milioni 192.6 kwa mwaka 2017, lakini kiasi cha Sh. milioni 107.1 kimerejeshwa hadi kufikia Septemba mwaka 2018 ikiwa ni sawa na asilimia 56 ya mikopo hiyo. 

“Kati ya deni sugu la Sh. milioni 83.5, kiasi cha Sh. milioni 43.2 kimetokana na walimu waliondolewa kazini kwa kukutwa na vyeti feki na wasiyo na vyeti vya kidato cha nne…bado chama kinafanya jitihada kuwatafuta walimu husika, ili kulipa fedha hizo,” alisema. 

Lyamuya alisema pamoja na changamoto hiyo, lakini chama hicho kwa kipindi cha miaka 20 ya kuanzishwa kwake tayari kimefanikiwa kutoa mikopo ya zaidi ya Sh. bilioni 27 kwa wanachama wake, huku baadhi ya mikopo ikihusisha elimu, biashara na dharura nyinginezo. 

Alisema deni hilo sugu limesababishwa pia na baadhi ya wanachama kustaafu kwa hiari wakiwa na miaka 55 bila kutoa taarifa katika chama, huku wakifahamu bado hawajalipa madeni yao. 

Alitaja baadhi ya mafanikio kuwa ni pamoja na kukua kwa mtaji wa wanachama wa kukopeshana kufikia Sh. bilioni 5.1, huku chama kikijitegemea kwa asilimia 100 kwa mtaji wake wa ndani, kutokuwa na migogoro na ununuzi wa kiwanja mtaa wa Majengo Manispaa ya Moshi. 
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad