Wananchi Afrika Kusuni Waandamana Kisa Makonda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wananchi Afrika Kusuni Waandamana Kisa Makonda
Wananchi nchini Afrika Kusini wameandamana mpaka ubalozi wa Tanzania, wakipinga kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kukataza vitendo vya ushoga na usagaji kwenye mkoa wake.


Wananchi hao ambao idadi yao haikujulikana kwa mara moja, pia wamemtaka Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuingilia kati suala hilo, ikiwezakana awape kibali wananchi hao (mashoga) ambao wametajwa kuwa maisha yao yapo hatarini, waweze kuishi Afrika Kusini.

“Rais Ramaphopsa, tunakuita ili utambue hali iliyopo sasa Tanzania, kunyanyaswa kwa haki za binadamu na uhuru wa binadamu, mwambie Makonda kuwa haukubali hiki kitu, tunakutaka uwape hifadhi watu hawa  wa Tanzania, ambao wapo katika hatari ya kuporwa uhuru wao, tunakutaka uchukue hatua kama katiba yetu inavyosema na kitendo chako cha kutetea haki za binadamu”, walisikika waandamani hao kwenye ujumbe wao.

Ikumbukwe kwamba hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alianzisha kampeni ya kukamata watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za nchi, lakini kitendo hiko kimekuwa kikipingwa na makundi mbali mbali ya haki za binadamu, wakisema ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad