Zitto Kabwe Azungumzia Kuondolewa Bungeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe amesema kuwa si kweli kwamba yeye ndiye Mbunge anayemsumbua zaidi Spika Job Ndugai kama alivyodai kwani amekuwa akifuata taratibu na kanuni bila kuvunja sheria.


Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT-Wazalendo ametoa kauli hiyo leo baada ya kuulizwa kuhusu maoni yake kufuatia kauli ya Spika aliyoitoa jana akidai kuwa Zitto ni mbunge anayempa tabu kutokana na kauli zake.

"Sijui kwanini Spika amesema vile kwani mimi simpi tabu, nasimamia haki na Spika afuate kanuni tu”, amesema Zitto.

Jana Januari 17 katika mkutano wake na wanahabari, Spika Ndugai amesema amekuwa akishindwa kumfukuza bungeni mbunge huyo wa Kigoma Mjini kwa kuwa ndiye pekee anayekiwakilisha chama cha ACT- Wazalendo.

"Ni kweli Zitto Kabwe ananisumbua sana lakini, ukisema umtoe Bungeni unawaza mtu mwenyewe yuko peke yake ukimsimamisha atawakilishwa na nani?. Unamuacha tu lakini wale wengine nafukuza tu maana wako wengi akikosekana kwenye mjadala atawakilishwa na wenzake, hebu nisaidieni Zitto nimfanyeje?, alihoji Spika Ndugai.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad