"Hii ni Aibu, Hatupendi Kufika Huko" - Majaliwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema tabia zinazoendelea kwa baadhi ya viongozi wa mkoani Kilimanjaro zinalitia aibu Taifa na kuwashushia hadhi wahusika.


Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumamosi akiwa mkoani Dodoma wakati akifungua mkutano wa siku moja kwa Wakuu wa mikoa unaolenga kujadili namna bora ya upatikanaji wa masoko ya madini nchini.

Waziri Mkuu amesema kwamba taarifa alizozipata kutoka mkoani Kilimanjaro ni kwamba viongozi walipigana ofisini na kubainisha kuwa hilo si jambo zuri huku akishangazwa na watu hao kushindwa kufuata maelekezo ya mkuu wa mkoa.

“Hivi kuna nini Kilimanjaro, eti mkuu wa mkoa tueleze, inakuwaje hivi karibuni tunaleta mawaziri wakazungumza kwa mapana na tukadhani kumetulia lakini ghafla tena watu wanapigana ngumi, hii ni aibu. Hatupendi kufika huko lakini msitulazimishe na mamlaka husika ziamue kuchukua hatua, si jambo jema, lazima mambo kama haya yasipewe nafasi kabisa.  "amesema Majaliwa.

Amesema lengo la uteuzi kwa viongozi ni kutakiwa kufanya mambo ambayo kiongozi wao anayafanya ikiwemo kushirikiana na viongozi na taasisi nyingine na kukaa pamoja na kujadiliana kuhusu rasilimali za nchi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad