Kesi Ya Halima Mdee Yapigwa Kalenda Hadi February 7

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kesi Ya Halima Mdee Yapigwa Kalenda Hadi February 7
Kesi inayomkabili, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee anayekabiliwa na shtaka la kutoa lugha ya matusi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kusikilizwa Februari 7, 2019.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita ameeleza hayo leo Jumatano Januari 9, 2019 mbele ya hakimu mkazi mkuu Salum Ally kuwa kesi hiyo ilipaswa kuendelea na ushahidi lakini hakimu husika yuko likizo.

"Kesi imekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini kutokana na hakimu husika kuwa likizo, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na ushahidi," amedai Wakili Mwita.

Baada ya kueleza hayo Hakimu Ally aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 7, 2019 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kuendelea na hatua ya ushahidi. Tayari mashahidi wawili wa upande wa mashtaka wameshatoa ushahidi katika kesi hiyo.

Katika kesi hiyo,  Halima anadaiwa kutenda kosa hilo, Julai 4, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni.

Mdee anadaiwa kumtukana Rais John Magufuli kwa kusema “anaongea hovyo hovyo , anatakiwa afungwe breki” kitendo hicho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad