Makonda ashangazwa na Bar kufungwa saa sita usiku

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makonda ashangazwa na Bar kufungwa saa sita usiku
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, amesema kuwa anaandaa utaratibu ili wafanyabishara mbalimbali, wakiwamo wa baa waanze kufanya kazi kwa saa 24.

Wakati akitangaza neema hiyo, Makonda pia ameeleza kushangazwa na utaratibu unaotumiwa na baadhi ya wamiliki wa nyumba za kulala wageni wa kudai vyeti vya ndoa, unaowafanya wakose mapato.

Makonda aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na vyombo vya ulinzi na usalama, wakuu wa wilaya, makatibu tawala, maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa mkoa huo, kuhusu mkakati wa kukusanya mapato bila kuwabughudhi wafanyabishara.

“Maana ya Jiji la Dar es Salaam kuwa Jiji la kibishara ni pamoja na kuwawezesha wafanyabishara kufanya kazi kwa saa 24. Kwa sasa baa zinafunguliwa hadi saa sita usiku lakini mpango wetu zifunguliwe muda wote ili serikali ipate mapato", amesema Makonda.

Makonda amesema kwa sasa sheria iliyopo inaruhusu biashara za baa kufanyika hadi saa 8:00 usiku tofauti na awali ilikuwa mwisho saa 6:00 usiku lakini kuna baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi wamekuwa wakiwasumbua wafanyabishara kinyume cha taratibu zilizowekwa.

“Mfanyabishara afanye biashara muda wote, kama usalama upo na hapigi muziki unaosababisha usumbufu kwa wengine, kwanza ni vizuri kwa sababu ni ishara ya kuwapo kwa usalama", amesema Makonda.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Makonda hwawatalewa usiku kucha na kushindwa kuwajubika asubuhi kazini?

    ReplyDelete

Top Post Ad