Polisi yakanusha unyama wa kutisha, Majambazi kuvamia gesti

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polisi yakanusha unyama wa kutisha, Majambazi kuvamia gesti
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekanusha taarifa iliyokuwa ikidai kuwa  “Unyama wa kutisha” Majambazi wavamia gesti, wabaka wahudumu na kupora fedha….baada ya kuwapa vinywaji na biskuti zenye....

Januari 24 mwaka huu  saa 06.00 asubuhi iliripotiwa taarifa kuwa huko katika Bar na nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Malema iliyopo maeneo ya Makunguru, Kata ya Manga, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya watu watatu waliofahamika kwa majina ya LUCY MWAPASI [36] Mhudumu na mkazi wa Mwanjelwa, CHRISTINA KIPESI [37] Mkazi wa Ituha na DICKSON ALLY [22] Mlinzi na Mkazi wa Makunguru waligundua kuibiwa simu zao za mkononi tano [05] na fedha taslimu za mauzo ya Bar na nyumba ya kulala wageni kiasi cha shilingi 701,000/= na watu wawili wanaowafahamu kwa sura.

Inadaiwa kuwa watu hao walifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na mmoja wapo alichukua chumba namba 11 ambapo aliishi hapo kwa siku tatu [03] hivyo kujenga mazoea ya karibu na wahudumu hao.

Januari 23 mwaka huu saa 23:30 usiku muda wa kufunga Bar ulipofika, walibaki wahudumu wawili huku mmoja akiwa wa Bar na mwingine wa nyumba ya kulala wageni na mlinzi ndipo watu hao walitoka chumbani kwao na kuwaambia wale wahudumu kuwa wanataka kuwapa offer ndipo walikubali na kuwanunulia juice ya azam na biskuti wahudumu hao, vitu ambavyo vinadaiwa kuwa na madawa yadhaniwayo ya kulevya na baada ya kula wote walianza kulegea na kulala na kupoteza fahamu na kisha watu hao kutekeleza adhima yao ya wizi.

Wahanga walipata msaada toka kwa wasamaria wema majira ya saa 09:00 asubuhi ambapo walipelekwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu. Kwa mujibu wa mganga wa zamu aliyewafanyia uchunguzi na kugundua kuwa wahanga hao watakuwa wamekula/kunywa chakula chenye sumu au kinywaji chenye sumu hivyo aliwapatia matibabu kuondoa sumu mwilini na baada ya siku moja waliruhusiwa kutoka Hospitalini baada ya kupata nafuu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad