Uongozi wa Simba Wamkingia Kifua Aussems Baada ya Kipigo cha Goli 5

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Uongozi wa Simba SC umefunguka Baada ya kichapo cha mabao 5-0 na AS Vita katika mchezo wao wa hivi karibuni wa  Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi pamoja na kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Bandari kwenye michuano ya SportPesa Cup na kusema kuwa bado wana imani na kocha Patrick Aussems hivyo mashabiki wapunguze jazba.

Simba katika mashindano matatu ambayo wameshiriki yote hawana uwezo wa kutwaa kombe kutokana na kutolewa mapema ikiwa ni pamoja na lile la FA, Mapinduzi waliishia fainali na kombe la SportPesa ambalo leo wanapigania nafasi ya tatu na Mbao FC.

Ofisa Habari wa Simba , Haji Manara amesema katika mkataba wa mbelgiji Aussems hakuna makubaliano juu ya makombe mengine zaidi ya kombe moja na sharti moja ambalo amelitimiza tayari.

"Kwenye mkataba wa Aussems tumemwambia kwamba tunahitaji atufikishe hatua ya makundi Afrika jambo ambalo amefanikiwa kulifanya na lipo kwenye mkataba pamoja na kutupatia ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao upo mikononi mwetu.

Hata hivyo amesema makombe mengine hawajayaweka kwenye makubaliano wanayoshiriki kulinda heshima na wakifanikiwa kuyapata ni jambo jema hivyo na kushindwa kuyapata kwao haina maana kwamba Kocha hafai hapana wanamipango yao na wanafanya kazi kwa utaratibu.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad