“Taarifa za Manchester United Kununuliwa na Mtoto wa Mfalme Saudia ni za Uongo” Waziri wa Habari Saudia Arabia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

“Taarifa za Manchester United kununuliwa na mtoto wa Mfalme Saudia ni za uongo” Waziri wa habari Saudia Arabia
Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman amekanusha madai kuwa anantaka kuinunua Manchester United kwa kitita cha pauni bilioni 3.8.


Tetesi ziliibuka mwishoni mwa wiki zikimuhusisha mwanamfalme huyo na kutaka kuinunua klabu hiyo tajiri nchini Uingereza.

Wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazers wanadaiwa kuwa hawana mpango wa kuiuza timu yao.

Wamiliki hao kutoka Marekani waliinunua Man United kwa kitita cha pauni milioni 790 mwezi Mei 2005
“Taarifa za Manchester United kununuliwa na mtoto wa Mfalme Saudia ni za uongo” Waziri wa habari Saudia Arabia
.


“Ripoti zinazomuhusisha Mwana Mfalme Mohammed Bin Salman kuwa anataka kuinunua Manchester United ni uongo mtupu,” amesema waziri wa michezo wa Saudia Turki al-Shabanah.

“Manchester United walifanya mkutano na mfuko wa uwekezaji wa umma PIF wa Saudia kuhusu nafasi ya udhamini. Lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa,” ameeleza waziri huyo.

Salman, 33, aliteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha Ufalme wa Saudia Juni 2017.

Chini ya utawala wake, taifa hilo limelaaniwa vikali kwa visa vya kukiuka haki za binaadamu na kushutumiwa kwa mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi katika ubalozi wa Saudia nchini uturuki mwaka jana.

Mwezi Oktoba mwaka jana, Manchester United ilijitoa kwenye mazungumzo na PIF baada ya mauaji ya Khashoggi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad