Trump atangaza mkutano mwingine na rais Kim Jong-un wa Korea kaskazini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Trump atangaza mkutano mwingine na rais Kim Jong-un wa Korea kaskazini
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza katika hotuba yake kwamba ataanda mkutano wa pili kujadili masuala ya nyuklia na kiongozi wa Korea kaskazini mwezi huu.

Katika hotuba kwa taifa iliyoambatana na kauli mbiu "Choosing Greatness", aliapa kwa mara nyingine kujenga ukuta mpakani.

Huku akihimiza umoja, kiongozi huyo wa Republican pia amesema jitihada za 'uchunguzi ulio na upendeleo' wa Democratic huenda ukaathiri ustawi wa Marekani.

Kwa ukali, wanachama wa Democrat wamemshutumu Trump kwa kupuuza maadili ya Marekani.

Hotuba hiyo kuu ya rais Trump imejiri baada ya pengo la muda mrefu kuwahi kushuhudiwa katika historia, la kusitishwa ufadhili kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.

Alichochea kufungwa kwa mashirika ya serikali kwa kuitisha ufadhili wa ukuta wa mpakani kati ya Marekani na Mexico na kuishia kubadili kauli hiyo baada ya wanachama wa Democrat kukataa wazi.

Trump amesema atakuna na Kim Jong-un huko Vietnam kuanzia Febrauri 27-28.

Mipango ya mkutano wa pili imekuwa ikipangwa tangu mazungumzo ya historia kati ya viongozi hao mwaka jana.

Mkutano wa Trump na Kim mnamo Juni mwaka jana huko Singapore ulikuwa wa kwanza kati ya rais anayehudumu wa Marekani na kiongozi wa Korea kaskazini.

Mnamo Jumanne usiku, Trump alisema: "Mateka wetu wamerudi nyumbani, majaribio ya nyuklia yamesitishwa na hakujakuwa na shambulio la makombora kwa miezi 15.

"Kama sikuchaguliwa rais wa Marekani, kwa maoni yangu tungekuwa katika vita vikubwa na Korea kaskazini hivi sasa.

"Bado kazi kubwa imesalia, lakini uhusiano wangu na Kim Jong-un ni mzuri."

Baada ya miaka miwili ya ufuasi wenye uhasama, Trump ameregelea wito wa umoja wa kisiasa ambao ameutoa katika hotuba zake mbili zilizopita za kila mwaka bungeni.

"Pamoja tunaweza kuvunja mkwamo wa kisiasa wa miongo kadhaa," amesema.

"Tunaweza kuziba migawanyiko ya siku za nyuma, tukaponya vidonda vya jadi, na kujenga muungano mpya."

Trump ameelezea maeneo ambayo yanaweza kufikiwa makubaliano, kama kuimarisha miundo mbinu, kupunguza bei za dawa na kupambana na saratani kwa watoto.

Lakini saa chache kabla ya hotuba hiyo, Chuck Schumer, kiongozi wa Seneti wa chama cha Democratic amemshutumu Trump kwa "kuidhinisha taifa lenye mgawanyiko" kwa sehemu kubwa ya mwaka.

Katika chakula cha mchana na waandishi habari kwenye ikulu ya White House Jumanne, Trump alimuita Schumer "muovu", na kutumia tusi, New York Times inaripoti.

Wakati Trump akitoa hotuba yake kwa taifa Jumanne usiku, mpinzani wake mkuu alikuwa amekaa nyuma yake.

Kiongozi wa Democrats katika bunge la wawakilishi, Spika Nancy Pelosi, aliidhinisha upinzani kwa matakwa ya rais kuhusu ufadhili wa ujenzi wa ukutana mara nyingi humkebehi.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad