Akamatwa na Vidumu vya Petroli Kanisani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Akamatwa na vidumu vya petroli Kanisani
Mwanaume mmoja amekamatwa baada ya kuingia kwenye kanisa la Mtakatifu Patrick jijini New York akiwa amebeba vidumu viwili vya Petroli , Polisi anaeleza.

Walinzi walimkabili mtu huyo mwenye miaka 37 alipokua akiingia kanisa la Manhattan siku ya Jumatano jioni.

Aliyamwaga mafuta chini kisha maafisa wakamkamata kumpeleka korokoroni.K

Naibu kamishna wa polisi John Miller amesema tukio hilo linaloshukiwa kuwa baya lilitokea siku mbili baada ya kanisa la Notre-Dame jijini Paris.

”Mtu alikua akitembea usawa wa kanisa amebeba magaloni ya mafuta, na vibiriti, ni jambo la kushukiwa”.Alisema Bwana Miller

Afisa wa intelijensia na masuala ya ugaidi amesema ni ‘mapema sana’ kueleza kama kusudio la mtu huyo ni kutekeleza vitendo vya kigaidi

Alipokabiliwa nje ya Kanisa, Mwanaume huyo aliwaambia maafisa kuwa gari yake iliishiwa mafuta na alikua akipita mbele ya kanisa hilo ili kulifikia.

Alikamatwa na polisi walitazama gari lake na kuona kuwa halikua limeishiwa mafuta. Haijulikani mtu huyo alikua na mipango gani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad