Mwakyembe Awataja Walio Ihujumu Serengeti Boys

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amedai miongoni mwa sababu za timu ya Serengeti Boys kufanya vibaya ni baadhi ya Mawakala wa wachezaji wa nchi za nje kuwaahidi baadhi ya wachezaji kiasi kikubwa cha pesa na kutakiwa timu kubwa.

Akijibu hoja ya Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia wakati wa mjadala wa Wizara hiyo aliyehoji kitendo cha Serengeti Boys kutofanya vizuri kwenye michuano ya AFCON chini ya miaka 17 kwa kuambuliwa kichapo katika mechi zote tatu walizocheza na kutupwa nje ya michuano.

Akihoji suala hilo Mbunge Mkamia amesema kuwa, "huwezi ukaandaa mashindano ukashika nafasi ya mwisho hata Korea aliishia robo fainali, nilishangazwa pale kamati ilipotangaza wakichukua ubingwa watawapa magari na milioni 20, ni sawa na mtoto wa miaka 8 ana birthday, unamwambia nitakununulia gari, hatukuiadaa timu vizuri hata mashindano waliofanya vizuri yalikuwa ni bonanza."

Akijibu hoja hiyo Waziri Mwakyembe amesema kuwa, "vijana wetu walikuwa na presha ya kuibeba Tanzania, pia nawalaumu Mawakala waliokuja  nchini wakina Diouf, Etoo waliwaambia watoto wadogo tunawahitaji kwenye timu yetu tutakulipa milioni 100, wakawa wanacheza kwa kuangalia zile hela. Baadhi ya  wazazi wakawaambia watoto wao wasicheze watavunjika mguu."

Bunge kwa sasa linaendelea jijini Dodoma ambapo leo hii ilikuwa ni kujadili makadirio ya bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad