Rais Tshisekedi na Kabila Wakutana Kujadili Uteuzi wa Waziri Mkuu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaendelea kusubiri kwa hamu na shauku kubwa uteuzi wa Waziri Mkuu mpya, miezi kadhaa baada ya Felix Tshisekedi kuchukua mikoba ya Joseph kabila kwenye uongozi wa nchi.

Wawili hao walikutana na kuzungumzia kuhusu nafasi ya Waziri Mkuu ambayo imesalia wazi, miezi minne baada ya uchaguzi wa urais uliompa ushindi Felix Tshisekedi na kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi.

Awali Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila walikuwa hawaelewani kufuatia mvutano wa kisiasa uliokuwa ukiikumba DRC na kisha baada ya uchaguzi wa urais wawili hao waliamua kufanya kazi kwa ushirikiano wakiwa katika muungano mmoja wa kisiasa.

Rais Tshisekedi na Joseph Kabila walikuwa hawajakutana kwa wiki kadhaa kutokana na ziara za kikazi za Tshisekedi. Lakini kwa pande zote mbili, wanahakikisha kuwa rais wa sasa na mtangulizi wake huzungumza mara kwa mara.

Mazungumzo kati ya wawili hao kuhusu uteuzi wa Waziri Mkuu na uundwaji wa serikali yalidumu kwa muda wa saa moja.

Kuhusu suala la Waziri Mkuu, mazungumzo yanaendelea, karibu miezi minne baada ya Felix Tshisekedi kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mwanzoni, wawili hao walikuwa wamechagua timu za mazungumzo, lakini mazungumzo yao yaliambulia patupu. Mazungumzo hayo sasa kuhusu uteuzi wa mtuu atajkayeshika wadhifa wa Waziri Mkuu yanafanyika katika ngazi ya juu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad