Polisi Wakatazwa Kuwashambulia Waandamanaji Sudan

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waandamanaji wanamshinikiza rais Omar Al-Bashir kuachia madarakaPolisi nchini sudan imewaamuru maafisa wake kutowashambulia maelfu ya waandamanaji waliopiga kambi nje ya makao makuu wa jeshi mjini Khartoum tangu Ijumaa.

Awali milio ya risasi ilisikika nje ya makao ya jeshi na ripoti zinasema kuwa maaskari wanaotoa ulinzi kwa waandamanaji wamepigwa risasi na maajenti wa serikali.


Katika taarifa yake msemaji wa polisi aliandika"Tunatoa amri kwa vikosi vyote" visiingilie "maandamano ya amani au kuwashambulia wananchi".

"Tunamuomba Mungu asaidie kuleta utulivu nchini mwetu... na kuwaunganisha Wasudan... na kufikiwa kwa makubaliano yatakayosaidia kupokezana madaraka kwa amani," iliendelea kusema taarifa hiyo.

Waziri wa mambo ua ndani wa nchi hiyo amesema waandamanaji saba waliuawa siku ya Jumatatu na wengine 15 kujeruhiwa, huku maafisa 42 wa vikosi vya usalama nao wakijeruhiwa pia.

Ameongeza kuwa karibu watu 2,500 wamekamtwa.

Mmoja wa wandamanani hao, Ahmed Mahmoud, ameimbia BBC kuwa maajenti wa kitaifa wa upelelezi walitumia mabomu ya kutoza machozi na risasi halisi dhidi ya waandamanaji.

Amesema maaskari wamewatengea eneo salama waandamanaji karibu na makao makuu ya jeshi la taifa.

"Hakuna haja ya Omar al-Bashir kutumumia majangili wake kutuondoa barabarani, hatuendi popote," alisema.

Mwandamanaji mwingine ameiambia BBC kuwa sio kila mwanajeshi ana unga mkono vugu vugu la maandamano; Maafisa wa ngazi ya juu jeshini wanaunga mkono serikali iliyopo madarakani, huku wale wa ngazi ya chini wakiunga mkono waandamanaji.

Image caption
Rais Bashir alitangaza hali ya hatari nchini Sudan mwezi Februari
Siku ya Jumatatu kuliibuka video inayowaonesha maafisa wakifyatua risasi kuelekea sehemu ambayo haikubainika huku waandamanaji wakijificha nyuma yao.

Waandamanaji walisema kuwa maafisa hao walikuwa wanajibu mashambulio kutoka kwa maajenti wa NISS.


Kumekuwa na miito ya kuitaka serikali ya Sudan kutotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia.

Marekani, Uingereza na Norway yametoa wito kwa serikali kutoa suluhisho la mpito la kisiasa.

''Ni vyema serikali ishughulikie matakwa ya wandamanaji kwa njia "ya uwazi na uwajibikaji", ilisema taarifa yao.

"Kutofanya hivyo kutasababisha machafuko. Mamlaka nchini Sudan ina jukumu la kuzua matukio kama hayo," iliendelea kusema taarifa yao..

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa pande zote mbili "kuwa na subira ili kuzuia kuzuka kwa machafuka".

Mwandishi habari Mohamed Ali Fazari, aliyekuwepo katika umati wa waandamanaji mjini Khartoum, anasema waanadamanaji hao wanaliomba jeshi lishirikiane na raia dhidi ya serikali.

Umati ulipiga kelele ukisema "uhuru, uhuru, haki - jeshi moja, watu wamoja", ameiambia BBC.

Kiini cha maandamano hayo awali kilitokana na gharama kubwa ya maisha lakini sasa ni ya kumshinikiza rais Bashir ambaye amekuwa madarakani kwa takriban miaka 30 sasa, ajiuzulu.

Uchumi wa Sudan umeathirika kwa muda mrefu na vikwazo vya Marekani kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita inayoishutumu Khartoum kwa kufadhili makundi ya kigaidi.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad