RC Makonda atimiza ahadi ya kuwapatia Wajane Milioni 10

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo ametimiza ahadi yake aliyoitoa juzi ya kuwapatia wajane kiasi cha Shillingi milioni 10 za kusaidia kutatua changamoto za kiofisi zilizokuwa zikiwanyima usingizi wajane ikiwemo ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwenye nyumba wanayoitumia kama ofisi.



Itakumbukwa juzi wakati wa kongamano la wajane RC Makonda alitoa ahadi ya kuwapatia milioni 10 na kuwatafutia eneo la kujenga jengo la ofisi za makao makuu ya chama cha wajane Tanzania na tayari eneo limepatikana tayari kwa ujenzi.

Mapema Leo Afisa elimu wa Mkoa wa Dar es salaam, Hamis Lissu amewakabidhi Milioni 10 kwa niaba ya RC Makonda ambae yupo katika majukumu mengine ya Kitaifa.

Kwa upande wao wajane wamemshukuru RC Makonda kwa kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili na wanaamini kupitia uongozi thabiti wa RC Makonda ujenzi wa jengo la makao makuu ya chama hicho utakamilika kwa uharaka.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad