Waganga wa Jadi Wanne Wakamatwa na Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waganga wa Jadi Wanne Wakamatwa na Polisi
Watu wanne ambao ni waganga wa jadi maarufu kama Rambaramba wanashikiliwa na jeshi la Polisi Wailayani Tabora mkoani Tabora kwa kuweka mazindiko katika Shule ya msingi Ndevelwa.

 Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Emmanuel Nley amesema watu hao walikuwa wanafanya mazindiko katika Shule hiyo ambapo wanafunzi walikuwa wanaanguka darasani.

“Hawa waganga maarufu kama kamchape au lambalamba wanafanya lamli na kuwaaminisha wananchi imani za kishirikina na kusababisha mauaji na migogoro katika jamii”, Amesema Nley.

Kamanda Nley amesema wameweza kuwakamata viongozi wa kijiji akiwemo Rashidi Ally Mwenyekiti wa kijiji cha Ndevelwa, Emmanuel Jacobo Mwenyekiti wa mtaa, Ramadhani Juma Mwenyekiti kamati ya wazazi Shule ya msingi Ndevelwa.

“Hawa viongozi wa kijiji walikubaliana kuwaita na kuwahifadhi waganga hawa ili kuzuia mapepo  yaliyokuwa yanawaangusha wanafunzi  darasani mbapo ni kinyume cha sheria”amesema Nley

Aidha amewataka wananchi mkoani humo kuachana na mila potofu na kuwaamini waganga wa jadi kwani ndio chanzo cha migogoro na kusababisha mauaji katika jamii.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad