Nandy Atishiwa Kuumbuliwa na Shabiki Wake, Aampa Block Instagram

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wasanii wengi na watu maarufu nchini huwa na mtu au watu mpaka watatu wanaomsaidia kumpigia debe katika mitandao ya kijamii haswa kuhusu mambo ya shows,kazi zao au hata mafanikio yao. Wengine hudiriki hata kutumia makampuni yanayohandle akaunti za mitandao ya kijamii.

Na mara nyingi watu hawa huwaga wako karibu sana na mastaa hao na huwa wanajua vitu vingi sana juu ya maisha yao. Na tatizo linakuja pale wanapoamuaga kutishia kumuumbua staa.

Malkia wa muziki wa Bongo flava nchini, Faustina Nandy Charles ama Nandy amegongana na moja ya promoter wake mtandaoni amabe alikua anashare picha zake za maevents mbalibali na kumsifia.

Cheki hizi kabla ya bifu


Siku ya jana kwenye instgram, shabiki huyo alimpa Nandy masaa 3 wawasiliane . Na alitishia kumwaga mtama kama hakidharau ombi hilo.Cheki;

By @the_originaleast
Wewe mwanamke nakupa 3 hours Uje DM kabla sijachafua khali ya hewa !!!!!Unakijua kichwa changu huwa sitabiliki !!!!! Nabadirikaga kama upepo wa bahari !!!!!!Na nikiwaga na hasira lazima nilimwage lote ndo nitulie so Jiheshimu Nandy !!!!! Narudia jiheshimu !!!!! .Nitaachia mapicha picha hapa nirudi kuwa the most hated page Hapa Instagram !!!!! Muulize Misa !!!



Baada ya Nandy kuona post hii alimblock shabiki huyo, na hili likazidisha hasira sana kwa shabiki huyo na kuandika


@the_originaleast
Hiki kitoto kinakiburi !!!!!! Kimenichukuliaje kwani 🤔🤔🤔🤔Nimekipa 3 Hrs kimenilamba block !!!!!! .Kumamake Sasa ndo Umenitibua mavuzi !!!!!! Ngoja nikalivute nirudi !!!!!nitamwaga yote kwanzia Msiba !!!! Mshenzi sana Huyu mtoto na bichwa lake ka bata maji !!!

Hali inanekana kuwa shwari sasa baada ya shabiki huyo kuomba msamaha kwa msanii kwa kudai kuwa aliambiwa maneno ya uongo na watu juu ya Nandy. Hili liwe fundisho kwa mastaa wengine nchini kwa kuwaamini watu kupita kiasi.

@the_originaleast
Dada Nandy @nandy_official_stylist !!!! Leo si jumapili ☹️☹️☹️ Si mmeenda Church !!! Si baba Mchungaji kafundisha Kusamehe !!!!! Sasa hii block imekaaje 😭😭 Nishaomba Msamaha private kwa kumuita bata maji 😩😩 Ni watu walinitumia umbea wa Uongo !!! . .  
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad