Ubovu wa VAR Ndiyo chanzo cha Esperance Kunyang’anywa Ubingwa wa Afrika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Klabu ya Esperance imetakiwa kurejesha kombe la ligi ya klabu bingwa Afrika pamoja na medali walizopewa na Shirikisho la Mpira wa miguu Afrika Caf huku kuwa tayari kwa kucheza mechi ya marudiano ya fainali.

Esperance ya Tunisia iliongoza kwa goli 1-0 kwenye mechi ya marudiano ya klabu bingwa Afrika lakini wapinzani wao Wydad Casablanca waliondoka baada ya goli lao la kusawazisha kukataliwa

Baada ya kukataliwa kwa bao lao, Wydad walitaka video ya wasaidizi wa waamuzi VAR kuthibitisha kama lilikua goli au la lakini mfumo wa mashine hiyo ulikua haufanyi kazi.

Shirikisho la soka Afrika (Caf) lilisema kuwa mechi ya marudiano itachezwa katika uwanja wa ugenini.

Matokeo hatimaye yalisimama kuwa 1-1 kutokana na mechi ya kwanza ya Morocco

Mechi ya marudiano itafanyika baada ya michuano ya kombe la mataifa Afrika itakayofanyika nchini Misri, itakayomalizika tarehe 19 mwezi Julai.

Taarifa ya Caf imesema ”taratibu za mchezo na usalama havikufuatwa” kwenye mechi ya marudiano na kuweka wazi kuwa wachezaji wa Esperance lazima warejeshe medali za ushindi na kombe.VAR

Wachezaji hawakujulishwa kama mashine ya VAR ilikua haifanyi kazi
Mchezo wa marudiano uliingia dosari baada ya Waydad kufikiri kuwa wamesawazisha dakika ya 59 kupitia goli la kichwa la Walid El Karti.Goli lilikataliwa kwa madai ya kuvunja sheria za mchezo.

Mashine ya VAR ilionekana kando ya uwanja lakini wachezaji hawakuelezwa kamailikua haifanyi kazi kazi.Esperance

Esperance ilipopata ushindi kabla ya ushindi kutenguliwa
Hatimaye mwamuzi akatoa ushindi kwa mabingwa mara tatu, Esperance baada ya dakika 95.

Rais wa Wydad amesema timu yake ”imeathirika” na Caf ikaitisha mkutano wa kamati kuu ambao walitoa uamuzi wa kuwepo kwa mechi ya marudiano
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad