Musiba Amvaa January Makamba adai Kufanya Ufisadi ya Sh Bilioni 1.5

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwanaharakati huru, Cyprian Musiba ameanika hadharani ufisadi wa Sh bilioni 1.5 anaodawa kufanya na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba.

“Naanza kuwachambua mmoja baada ya mwingine naanza na huyo mtakatifu January Makamba ambavyo sio mwadilifu na ni miongoni mwa waliofanya ufisadi katika nchi hii,” alisema Musiba.

Aliongezea kuwa:“Kwa sababu ni mtoto anatoka sehemu wa watoto wa viongozi unaachwa unakula bata sasa utaratibu huo haupo iwe ni mtoto wa maskini ama tajiri wote wana haki ya msingi,” alisema Musiba.

Alisema makamba ana kampuni yake iliyoitwa Bombuli ilisajiliwa mwaka 2010 na kampuni yake ilipewa mkopo wa Sh bilioni moja  katika kipindi cha miaka mitano mpaka sasa imerejesha Sh million 100.

“Mapungufu yalijitokeza katika huo mkopo huo kiasi cha juu cha mkopo kilitakiwa apatiwe Sh milioni 150 na kati ya Sh bilioni moja sehemu ya riba iliyorudishwa ni Sh milioni 100 fedha ambazo ni za wastaafu,” alisema

Aliongezea kuwa:”Leseni ya biashara ilisajiliwa Ilala na sio Luthoto lakini watu wapo Luthoto.
Mpaka juni 2019  deni limefika Sh bilioni 1.5. Sh milioni 289 ni riba na 259 ni tozo alizichukua fedha hizo kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya kugombea urais.

“Angekuwa amechukua mwananchi wa kawaida angekuwa Segerea ni sababu gani NSSF inashindwa kwenda Takukuru kumpeleka January Makamba afikishwe mahakamani. Mahakama na mahabusi zipo kwa ajili ya familia maskini tu? Sababu gani inafanywa huyu mwizi asipelekwe mahakamani?,” alihoji Musiba.

Musiba alisema yeye akiwa kama mwanaharakati huru anaomba Watanzania wamuelewe sio kwamba anatukana watu haya mambo hayakuwa ya kawaida kwa sababu ukiwa CCM ama mtoto wa kigogo hauguswi.

Alisema hajawahi kutukana mzee yoyote anazungumzia ufisadi uliofanywa na wazee jinsi walivyoizalilisha nchi.

Musiba alisema fedha zingetumika katika shughuli za maendeleo kama kujenga madarasa ya shule, hospitali na kusaidia wajawazito ama shughuli nyingine.

“Jambo jingine linalomuhusu Makamba wakati akiwa Forest anasoma kuna rafiki yake alipigwa risasi kwa ujambazi. Naomba January ajibu huyo Sizy alikuwa rafiki yake au sio rafiki yake ni kwa nini aliuawa na yeye kuhamishwa shule kupelekwa nje ya nchi kuna watu wanataka kuwa Rais kuja kutuvurugia nchi yetu jambazi unataka kuwa Rais haya ni mambo ya aibu kabisa,” alisema

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hizi tuhuma tuna mwachia BW. Diwani
    na huki Ninja na Siroo wakiwa chonjo.

    Watu wanashindwa kupata Vikokoto kumbe Mafisadi tumewabeba kwa kutumia majina ya baba zao.

    Na wengine wana wafata wale wa Barriki kwao Accasia .

    Hapana na Dau na Jitto pia ndani...!!?

    Hongera mwana Harakati Musiba.
    Endelea kutumegea tuyafanyie kazi katika awamuya HAPA KAZI TU..!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad