AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Uamuzi huo umetolewa jana na Prof.Mbarawa baada ya kupokea taarifa za kutokamilika kwa mradi huo kutokamilika kwa wakati huku wakiendelea kutoa ahadi za uongo.
Mbarawa amefafanua kuwa Wakandarasi hao wameshindwa kutimiza mashariti ya mkataba walioingia na serikali hivyo hawatakuwa na nafasi tena ya kuendendelea kutokamilisha mradi huo licha ya kuwa fedha wameshalipwa na serikali.
Amesema serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais, Dk John Magufuli haitakubali kuendelea kuwakumbatia wakandarasi wazembe ambao wanakwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi katika maeneo wanayoishi.
Kwa upande wake Ezekiel Maige ni mbunge wa jimbo la Msalala amemuomba Waziri Mbarawa kuwabana wakandarasi hao ili mradi huo ukamilike kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kupata maji safi na salama.
Nao baadhi ya wananchi Kurwa Kitunga na Kashindye Singu wa Kata za Mwakata na Mwendakulima waliojitokeza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Waziri huyo wameomba kujengewa magati ya maji katika vijiji ambavyo kunashida ya maji ili kuwawezesha kuacha kutumia maji ambayo sio safi yanayotumika pamoja na wanyama.
Kampuni zilipewa dhabuni ya kujenga mradi huo ni pamoja na Oriental conslin limited na Changs ambazo zimepewa kandarasi hiyo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 22 ambapo walitakiwa kukamilisha mradi huo mwezi june mwaka huu.
Bado Waziri Mbarawa anaendelea na ziara yake ya kikazi ya siku 4 mkoani shinyanga kukagua miradi mbalimbali ya maji.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK