Takukuru yataka wajumbe wa ardhi wapewe elimu kupunguza malalamiko

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Ruvuma, Yustina Chagaka ameitaka idara  inayoshughulika na masuala ya ardhi mkoani humo kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wajumbe waliopo katika mabaraza ya ardhi ili kupunguza malalamiko.

Wito huo umetolewa na mkuu huyo ofisini kwake, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji ya robo mwaka kwa waandishi wa habari.

Alisema idara ya ardhi, inaongoza kulalamikiwa na wananchi mbalimbali  na kumekuwapo viashiria vya mianya ya rushwa.

Alisema utendaji kazi wa robo ya mwaka, kumekuwapo na malalamiko mengi yanatoka sekta ya ardhi ambayo hadi sasa yamefika 17.

Alisema migogoro inayoshughulikiwa na mabaraza ardhi ya vijiji na kata,wajumbe wake wengi wameteuliwa kushughulikia migogoro hiyo huku hawana elimu ya utambuzi kuhusu masuala ya ardhi.

Alisema baadhi ya wajumbe, wanatumia nafasi hiyo kujipatia vipato kwa walalamikaji kwa kuwaambia watoe gharama za kwenda maeneo ya migogoro  ambako mwisho wa siku anayetoa kiasi kikubwa ndiye anayeonekana mwenyewe haki.

“Ofisi yangu imepata malalamiko mengi kutoka idara hii, tumejipanga kupambana nalo kisawasawa haiwezekani migogoro imekuwa mingi mno eneo hiuli,”alisema Chagaka.

Alisema idara zingine zinazolalamikiwa na idadi ya malalamiko katika mabano, ni elimu (10), halmashauri (7),Serikali za mitaa (5), polisi (5),vyama vya ushirika (4), mahakama (4), maji (3) na taasisi za fedha (2). Kuhusu miradi ya maji, alisema kwa  asilimia kubwa imekuwa na matatizo kukamilika
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad