Waziri Jenista aipongeza TCC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama  ameipongeza Kampuni ya Sigara Tanzania TCC, kwa kutekeleza Sheria ya kazi baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya hali bora kazini ili kuimarisha na kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo  iliyofanyika Jijini Dar es Salaam kati ya Kampuni ya sigara TCC na Chama cha Wafanyakazi Viwandani,Biashara na Taasisi za Kifedha (TUICO), Waziri Jenista alieleza kufurahishwa kwake na kampuni ya TCC kwani imezingatia na kutekeleza sheria Namba .6 ya mwaka 2004 ya  Ajira na Mahusiano kazini  na kanuni zake za mwaka 2007.

“Sheria namba 6. ya mwaka 2004 pamoja na kanuni zake zimeweka muongozo wa utaratibu na njia za kufuatwa pamoja na masuala muhimu ya kuzingatia katika kufanya majadiliano mahala pa kazi, ili kudumisha uhusiano na hii ilifanyika kwa TCC na ni jambo jema sana tunawapongeza kutekeleza Sheria”, Alisema Waziri Jenista.

Waziri Jenista alisema kuwa katika kutekeleza matakwa ya Shirika la Kazi Duniani, ILO, Serikali iliweka kifungu hiki kwenye sheria zake ili kuwezesha kuwepo kwa usawa kati ya mwajiri na mfanyakazi,  kwa hiyo TCC na TUICO  wamefanya kazi nzuri itakayowezesha motisha na ari kubwa kwa wafanyakazi.

Aidha Waziri Mhagama alisema kuwa utaratibu wa kuwepo na mikataba ya mahusiano mahala pa kazi umeanza mara moja baada ya uboreshwaji wa Sheria za kazi na ajira na, TCC haikuwa nyuma mara baada ya sheria hiyo kuanza kwani mpaka sasa mkataba wa hali bora mahala pa kazi unatekelezwa na unategemea kuisha mwaka 2020 na kuruhusu makataba mpya uliosainiwa leo kuingia kazini.

Waziri Jenista  aliipongeza  timu iliyofanya majadiliano na kuwezesha kuwepo kwa mkataba uliosaniwa leo, kwani unakidhi Sheria ya Wafanyakazi na maslahi yao mahala pa kazi hususani kwa wakinamama wenye watoto.

“Mkataba huu wa sasa umelenga zaidi katika kutoa maslahi ya wafanyakazi wote wa TCC, hongereni sana timu iliyoongoza majadiliano na kufikia muafaka, nimefahamishwa kuwa wakina mama wanaonyonyesha wataruhusiwa kwenda Nyumbani na kupewa posho ya Shilingi 5,000 kila siku ili wawahi kunyonyesha watoto wao katika kipindi chote cha kuhudumia watoto wao kama Sheria ya Kazi na ajira inavyoeleza hongereni sana”, Alisema Waziri Jenista.

Alisema kuwa katika utekelezaji wa Sheria hiyo, TCC wameenda mbali zaidi kwa kuwajali wakina mama wenye watoto njiti, ambao  watapewa ruhusa ya kulea watoto wao huku likizo ya uzazi ikihesabiwa kuanzia pale ambapo  mtoto angezaliwa.

Alisema kuwa wakina baba mkataba huo umejikita zaidi kuwapa fursa ya likizo ya siku 10 baada ya wake zao kujifungua, lakini pia makataba huo umegusa moja kwa moja wafanyakazi wa TCC kulipiwa ada za watoto wao kiasi cha shilingo 9,000,000 kwa mwaka na aliwataka wafanyakazi watumie hela hiyo kusomesha watoto wao na sio kwa matumizi mengine.

Waziri Mhagama alitoa rai kwa waajiri wengine kuiga mfano wa TCC wa kuwajali na kuwathamini wafanyakazi mahala pao pa kazi ili kuongeza ari ya kufanya kazi na kuimarisha uzalisha wa bidhaa utaowezesha nchi kupata mapato.

Aidha Waziri huyo wa Kazi alisema kuwa TCC ni moja ya kampuni ambayo inatekeleza kwa vitendo Sera ya Awamu ya Tano ya kuijenga Tanzania ya Viwanda kwani mkataba huo utaongeza nguvu ya kujituma kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Kwa upande wake Katibu Mkuu, TUICO, Boniface Mkakatisi alisema kuwa kampuni ya Sigara Tanzania inamahusiano mazuri na wafanyakazi wake ndiyo maana wameweza kufikia makubaliano hayo ambayo yana tija kwa pande zote mbili.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad