Fatma: Ile Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kuhusu janga la moto imeishia wapi?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Wakili wa kujitegemea Fatma Karume amehoji ile tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusiana na janga la moto iliyotokea mkoa wa Morogoro imeishia wapi.

Fatma aliandika ujumbe huu kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa  ” Ile Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kuhusu janga la moto # Morogoro imeishia wapi? Nawaza tu,”



Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa aliunda tume ya kuchunguza ajali ya lori la mafuta lililopinduka mkoani Morogoro kubaini kama kuna mamlaka zilishindwa kuwajibika baada ya lori la mafuta kupata ajali.

Majaliwa alisema tume hiyo inaanza kazi  na kumpatia ripori ndanj ya wiki ili kuchukua hatua.

“Manispaa kuna kitengo cha zimamoto japo najua walikuja kwa kuzima je walikuja baada ya muda gani? Tumesisitiza umakini na uwasibikaji nasikia tumeokoa mafuta sasa tumeokoa yakiwa yameisha? Nitaunda tume wanijibu haya maswali madogo,” alisema Waziri Mkuu.

Aliongezea kuwa:” Je huo muda ambao walikutana hawa ndugu zetu waliotangulia mbele za haki kwa ajili ya kutoa mafuta ni nani aliwazuia? mimi ninajua trafiki huwa wanakuwa na haraka sana ajali inapotokea nani alihusika kuwazuia,” alihoji Majaliwa
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Anti Fatuma, umedamshi Damshi...!!!
    kichuna chuna mwenyewe.

    langi nzuri ya njano sijui ni Cucci au luisi vitoni manake kama ingekuwa chama basi ni kama baba na Ammy.

    Au Yanga Dam Damu.

    ReplyDelete

Top Post Ad