Japan Yaadhimisha Miaka 74 Tangu Shambulizi la Marekani la Bomu la Nyuklia Huko Hiroshima

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Japan yaadhimisha miaka 74 tangu shambulizi la Marekani la bomu la nyuklia huko Hiroshima
Japana leo imeadhimisha miaka sabini na nne ya lile shambulizi la Marekani la bomu la atomiki katika mji wa magharibi wa Hiroshima huku maelfu ya watu wakihudhuria hafla hiyo ya kila mwaka.

Washiriki wakiwemo wahanga wa shambulizi hilo, vizazi vyao na wawakilishi wa kigeni walikaa kimya kwa dakika moja ilipotimu saa mbili na robo kwa saa za Japan.

Huo ndio muda ambao Marekani iliangusha bomu hilo la atomiki la B-29 katika mji huo miaka sabini na nne iliyopita Vita vya Pili vya Dunia vilivyokuwa vinaelekea mwisho wake.

Shambulizi hilo la bomu la nyuklia ambalo halikutarajiwa liliwauwa makumi kwa maelfu ya wakaazi kwa sekunde chache tu na mwishoni mwa mwaka huo watu 140,000 walikuwa wamefariki dunia kutokana na bomu hilo.

Siku tatu baadae Marekani iliangusha bomu jengine la atomiki katika mji wa Nagasaki ulioko kisiwa cha Kyushu. Mnamo Agosti 15 mwaka 1945 majeshi ya Japan yalisalimu amri na kufikisha mwisho vita hivyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad