AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Hii ni kufuatia tamasha la watani wao wa jadi Yanga maarufu kama 'Wiki ya Mwananchi' kuhitimishwa, Agosti 4 kwa ufanisi mkubwa pamoja na mchezo dhidi ya Kariobangi Sharks na kutoka sare ya bao 1-1.
Mashabiki wa Simba wakiongozwa na Msemaji wao, Haji Manara wana deni la kulipa kwa Yanga hii leo kwa kuujaza uwanja, kwani waliwacheka Yanga wakisema kuwa licha ya kujaa uwanjani lakini bado kulikuwa na mapengo mengi yaliyoonekana.
Deni la pili kubwa ni la matokeo uwanjani, ambapo katika mchezo wa Yanga na Kariobangi, mashabiki wa Simba walikuwa upande wa Kariobangi na wakionekana kuponda kiwango cha Yanga. Leo hii ni zamu yao wakihitaji kupata ushindi ili kusawazisha mambo.
Simba itacheza na Power Dynamos ya Zambia jioni ya leo. Kuelekea mchezo huo, Haji Manara amesema kuwa mashabiki watarajie mambo mengi ya kushangaza uwanjani, ikiwa ni pamoja na utambulisho wa mchezaji mmoja mpya na wa mwisho.
Pia amejigamba kuwa wao Simba ndiyo waanzilishi wa tukio hilo kwa vilabu hapa nchini kwahiyo wanataka kulifanya kwa namna nyingine. Tusubiri kuona kama Simba wataweza kujibu maswali hayo makubwa mawili hii leo.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK