Moto Wateketeza Watoto wa Familia Moja Ukerewe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Watoto watatu wa familia moja wakazi wa kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe wamefariki baada ya chumba walichokuwa kuungua kwa moto.

Watoto hao ni ni Rea Crizant (5), John Kamugisha(3) na Veronica Baraka (2).

Taarifa iliyotolewa jana Jumamosi Agosti 24, 2019 na katibu tawala wa wilaya ya Ukerewe, Focas Majumbi inaeleza kuwa tukio hilo limetokea jana Ijumaa saa 10 jioni katika kitongoji cha Ebugwe.

Mganga mkuu wa kituo cha afya Bwisya, Dk Joakimu Kole amesema watoto hao walifikishwa katika kituo hicho saa 11 jioni  lakini kutokana na kuungua kwa kati ya asilimia 65 hadi 100, wote walifariki dunia.

Amesema jitihada za kuwapatia matibabu zilifanyika kwa kiwango kikubwa lakini ilishindikana.

Mkuu wa kituo cha polisi Ukara, Joseph Paul akithibitisha tukio hilo, amesema uchunguzi wa awali unaonyesha moto huo ulitokea  baada ya mmoja wa  watoto hao kuwasha moto kwa kutumia kiberiti na ukashika nguo, godoro na chandarua.

Mwananchi
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad