Paul Makonda Aziomba Mamlaka Kumshughulikia "Makonda Feki"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka mamlaka husika kuchukua hatua za kisheria kwa anayehusika na uhalifu wa kimtandao wa kutumia jina lake kwenye ukurasa wa Twitter.

Makonda ametumia ukurasa wake wa Instagram kukanusha kuhusika na taarifa inayosambazwa katika mtandao huo juu ya wanaolaghai wanawake na kudai kuwa hana akaunti kwenye mtandao wa Twitter wala Facebook isipokuwa Instagram kwa jina la Baba Keagan.

“Naomba kuutaarifu umma kwa mara nyingine tena. Mimi Paul Makonda Mkuu wa Mkoa sina A/c TWITTER hata FACEBOOK. Mtu anaetumia jina langu ana malengo mabaya tena Kwa faida iliyojaa uovu.”

“Naziomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua kwani kunasiku atatoa kauli itakayoleta taharuki katika jamii. A/c pekee ni nayo tumia ni ya Instagrame tena Kwa jina la baba_keagan.”



#DizzimUpdates: Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda amezitaka mamlaka husika kumchukulia hatua za kisheria anayehusika na uhalifu wa kimtandao wa kutumia jina lake kwenye ukurasa wa twitter. Mhe. Makonda aliutumia ukurasa wake wa Instagram, pia kukanusha kuhusika na taarifa inayosambazwa mtandaoni huo juu ya wanaolaghai wanawake na kudai kuwa hana akaunti kwenye mitandao ya kijamii isipokuwa Instagram kwa jina la @baba_keagan. Written By @PresenterDMike.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad