Watu mashuhuri Tanzania watoa pole kufuatia ajali ya Lori la mafuta

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu mashuhuri Tanzania watoa pole kufuatia ajali ya Lori la mafuta

Baada ya watu kuungua moto na kupoteza maisha baada ya gari la mafuta kulipuka na kuwaka moto Msamvu Itigi mkoani Morogoro. Watu mashuhuri Tanzania watoa pole kufuatia ajali hiyo;

"Tumepokea kwa masikitiko taarifa kuhusu ajali ya lori la mafuta,  Morogoro, iliyosababisha moto na kuunguza watu kadhaa. Mkuu wa Mkoa na timu za uokoaji wanaendelea kukabiliana na  hali katika eneo la tukio. Taarifa kamili kuhusu idadi ya vifo na majeruhi itatolewa badae," Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi.

"Nimepokea kwa Mshtuko  Mkubwa ajali mbaya ya MOTO iliyotokea Msamvu Morogoro na kusababisha VIFO na MAJERUHI wengi!! Pole sana kwa ndugu, jamaa na marafiki.  Pole sana kwa Mkoa wa Morogoro na Taifa kwa MSIBA HUU MKUBWA. Mungu awapumzishe kwa AMANI!😭😭!," ameandika Halima Mdee.

"Nina toa  pole kwa msiba mkubwa uliotokea huko Morogoro kwa ajali na kulipuka kwa gari la mafuta na kusababisha vifo/vilema.Natoa wito kwa Mamlaka za Serikali kuchukua hatua kwa Polisi/Fire Morogoro,kwa uzembe mkubwa ktk kusimamia ajali ya aina hii haswa baada ya kuwa imetokea," Lema.

"Poleni Sana Ndugu Zetu Wa Morogoro kwa msiba huu mzito. Mungu Azilaze Roho Za Marehemu Wote Mahali Pema Peponi. Amen," ameandika Jokate Mwegelo.

"Poleni saa Ndugu zangu wa MOROGORO...Mwenyez Mungu azipe nguvu Familia zote katika kipindi hiki kigumu kwao, awaponye haraka majeruhi wote na kuzilaza roho za Marehem mahala pema peponi Amin," Diamond Platnumz.

"Mungu azilaze roho za ndugu zetu mahali pema peponi," ameandika Shilole.
"Nawaombea waliotangulia mbele za haki pumziko la milele na majeruhi wapone haraka," ameandika Bdozen.

"Nimepokea taarifa ya ajali huko Msamvu, Morogoro kwa mshituko mkubwa sana. Hiki ni kipindi kigumu na kisichoweza kuelezeka, pole kwa watanzania wote, ndugu, jamaa na marafiki. This is a total loss to the Families and nation at large. My deepest condolences," ameandika Hamisa Mobetto.

"Tuwaombee na Majeruhi wote wa ajali hii kubwa wapone haraka," ameandika Haji Manara.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad