Afisa Usalama Adakwa na Madawa ya Kulevya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya nchini inamshikilia aliyekuwa Afisa Usalama wa shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe kwa tuhuma za usafirishaji wa madawa ya kulevya kwa njia ya posta.


Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 23 na Kaimu kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji, ambapo amesema kuwa mwanaume huyo walimkamata kwa kushirikiana na jeshi la polisi na kwamba hapo awali aliwahi kutoweka kufuatia mahojiano yaliyokuwa yakiendelea dhidi yake.

''Mamlaka imemkamata George Mwangabe pamoja na wenzake sita wanaohusishwa na dawa za kulevya aina ya Heroin ambapo hadi sasa uchunguzi umekamilika na washtakiwa watafikishwa mahakamani'', amesema Kaimu Kamishina Kaji.

Kwa upande mwingine katika kipindi cha mwezi Septemba, Mamlaka hiyo imefanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya Heroin zaidi ya kilo moja katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza pamoja na zaidi ya kilo 214 za vifurushi vya dawa za kulevya aina ya mirungi, zilizokuwa zikisafirishwa kwa njia ya Posta kutoka Arusha kwenda nchini Uingereza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad