JPM Amteua Diwani Kuwa Mkurugenzi Mkuu Usalama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba.
 
 
Rais wa Tanzania, John Magufuli amemteua na kumuapisha Diwani Athuman kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuchukua nafasi ya Dk Modestus Kipilimba.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Kamishna Diwani Athuman Msuya mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Septemba 12, 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa uteuzi wake umeanza leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba
Kabla ya uteuzi huo, Diwani aliyeapishwa Ikulu, Dar es Salaam leo alikuwa mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba
Akizungumza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Kapilimba atapangiwa kazi nyingine.

Kamishna wa Polisi Diwani Athumani aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Septemba 6, 2018, nafasi aliyoitumikia kwa mwaka mmoja na siku 6. Kabla ya kwenda TAKUKURU alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) wa Mkoa wa Kagera.
Nafasi alizoshika Kamishna Diwani Msuya tangu 2015: ⭕️2015: Kaimu Kamishna wa Kamisheni ya Intelijensia ya Jinai
⭕️Mei 2015: Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)
⭕️Nov. 2016: Katibu Tawala Kagera
⭕️Sep. 2018: Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU
⭕️Sep. 2019: Mkurugenzi Mkuu TISS
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad