Mabeste Aeleza 'issue' ya Kukimbiwa na Mke Wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 
Rapa Mabeste ameeleza juu ya kile kinachoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu taarifa za kukimbiwa na mke wake “Mama Kendrick”.


Taarifa zinadai kuwa Mabeste amekimbiwa na mke wake kwa sababu ya shida na matatizo na sasa hivi yupo mjini Moshi akiwa na mwanaume mwingine.

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital Mabeste amesema hajui kinachoendelea kuhusu hilo na hata yeye ameona taarifa hizo katika kurasa za habari za udaku na mitandao ya kijamii.

“Inawezekana ila sijajua kwa sasa hivi, ikifikia hatua ya kutengana watu watajua na hata wasipojua ni sawa kwa sababu katika maisha, kutengana na kuanzisha mahusiano mengine ni moja ya maisha ni vitu vya kawaida”, amesema Mabeste.

Mabeste ameendelea kusema kuwa suala hilo halina ukweli wowote na hata akikimbiwa ni sawa tu hatakuwa wa kwanza kufanyiwa hivyo kwa sababu wapo wengi waliokimbiwa na wapenzi wao na maisha yakaendelea na lolote litakalokuja mbele yake atashukuru na ataendelea mbele.

Aidha ameeleza kuwa alijitoa kuhangaikia maisha ya mke wake kipindi alipokuwa na matatizo ya maradhi, alifanya vile kwa sababu ya upendo na majukumu kama mtu wake wa karibu na wala ahitaji fadhila yoyote.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad