Mahakama Yaelezwa Erick Kabendera Anaumwa Mguu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mahakama yaelezwa Erick Kabendera anaumwa mguu
Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili mwandishi wa habari nchini, Erick Kabendera umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa mteja wao bado anaumwa mguu wa kulia kwani umepooza na anashindwa kutembea vizuri.

Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari za ndani na nje ya Tanzania alifikishwa  Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu, ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh173.2 Milioni

Leo Alhamisi Septemba 12,2019, wakili  wa utetezi, Jebra Kambole amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Agustine Rwizile baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali Wankyo Saimon kueleza upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

“Mteja wetu ni mgonjwa mpaka sasa anashindwa kutembea vizuri mguu wa kulia umepooza na anashindwa kupumua vizuri hasa usiku.”

"Mteja wetu angepata vipimo vizuri, tunaiomba Mahakama kuielekeza idara ya magereza wampe fursa ya kupatiwa matibabu hospitali yoyote ya serikali na sisi mawakili tujue anaumwa nini," amedai  Wakili Kambole
TAZAMA WIMBO MPYA WA ROSA REE

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad