Mwalimu mbaroni ubakaji wa mwanafunzi ofisini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


JESHI la polisi Mkoa wa Mara limemkamata mwalimu wa Shule ya Msingi ya Bwai A, Lazaro Mmanga kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi (jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) wa mika 14, darasa la saba.

Habari ambazo zilifikia gazeti hili zilidai kuwa mwalimu huyo aligutukiwa na marafiki wa mwanafunzi anayedaiwa kufanya naye tendo hilo baya.

“Ni kwamba wanafunzi wale baada ya kuona mwenzao akiingia chumbani kwa kupitia dirishani, walikwenda kuchungulia na kuona kila kitu,” alisema mtoa habari wetu kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini ambaye aliongeza kuwa suala hilo tayari lipo polisi.

Alisema, wanafunzi hao walikwenda kuripoti tukio hilo kwa viongozi wa serikali ya kijiji ambao walifika haraka na kukuta mwalimu akiwa bado yupo ndani na denti huo, hivyo kuitwa polisi.

Akithibitisha habari hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Juma Ndaki alikiri kutokea kwa tukio hilo lilitokea Septemba 4 mwaka huu.

“Mwalimu huyo aliumbuliwa na wanafunzi waliokuwa wanamwagilia bustani katika eneo la shule hiyo ambao walimshuhudia akimficha mwanafunzi wake huyo katika ofisi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo.

“Wanafunzi hao walisema walimshuhudia mwalimu huyo akimpitisha mwanafunzi mwenzao dirishani na baada ya muda kutoka nje na kisha kumfungia ndani ya ofisi hiyo ambapo baada ya wanafunzi hao kuona tukio hilo walikwenda moja kwa moja kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali za kijiji eneo hilo,” alisema kamanda.

Kamanda Ndaki alisema, uongozi wa kijiji ulilitaarifu jeshi la polisi ambapo kwa haraka walifika shuleni hapo na kufanikiwa kumkamata mwalimu huyo na kumfikisha katika Kituo cha Polisi cha Mgango.

Kamanda Ndaki alisema kuwa, kabla ya kufanikiwakumtia mbaroni mwalimu, kumtia mbaroni mwalimu, askari hao walikuta umati mkubwa uliokuwa umezingira ofisi hiyo ya mwalimu mkuu wakizuia askari wasimkamate mwalimu huyo aliyekuwa ndani kwani walikuwa wamekusudia kumuua. “Askari polisi hao walipambana na wananchi waliowazuia kumtia mbaroni mtuhumiwa wakitaka kumuua, walirushia mawe gari la polisi lenye namba za usajili PT 1441 Toyota Land Cruiser na kuliharibu,” alisema kamanda.

Akifafanua zaidi Kamanda Ndaki alisema katika hatua za kuokoa gari hilo jitihada zilifanyika baada ya askari polisi kurusha risasi hewani kutawanya watu lakini kutokana na wingi wao, walijaribu kuchoma moto gari hilo lakini baadhi ya raia wema na askari polisi walifanikiwa kuuzima kabla ya kuleta madhara. Kamanda Ndaki alitaja uharibifu uliotokea kwenye

gari hilo kuwa ni lilipasuliwa kioo cha mbele na kubonyezwa bodi ambapo pia watu hao walivunja ofisi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo na kuharibu meza, madirisha na samani zingine ambapo haijajulikana thamani zake. Alisema upelelezi wa tukio hilo unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atapelekwa mahakamani, huku akiwaonya wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi.

Wakati huo huo jeshi la polisi limewakamata watu wawili kwa kosa la kupatikana na injini za boti 10, mali zinazodhaniwa za wizi baada ya kufanyika misako maeneo mbali mbali katika Wilaya za Musoma, Bunda, Butiama na Serengeti tangu Agasti 29 hadi Septemba 5 mwaka huu mkoani hapa.

Kamanda  Ndaki aliwataja waliokamatwa  na mali hizo kuwa ni  Walagai Masoya maarufu Nyajirali aliyekamatwa Septemba tatu mwaka huu katika maeneo ya Bwai  na ni Mwinyi Eunyo aliyekamatwa Septemba 3 mwaka huu akiwa na injini sita za boti. Kamanda ndaki alisema kuwa watu hao wanaendelea kushikiliwa na uchunguzi wake unaendelea kufanyika ili hatua za kisheria zichukuliwe
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad