Mwigizaji Mwala Aua Mtu, Atupwa Jela Kenya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Kabla ya uamuzi kutolewa na hakimu Adalo, Mwala aliiomba msamaha familia ya marehemu na kusema hakutenda kosa kwa kukusudia.

Mwigizaji wa Kenya Davies Mwabili maarufu kama Inspekta Mwala, kwa mara nyingine tena amejikuta kwenye matatizo ya kufungwa jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kumgonga na kumuua mpita njia eneo la Kaloeni, kaunti ya Kilifi.

Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa kituo cha polisi cha Kilifi Patrick Okeri alisema kwamba Mwabili alimgonga mwanamme huyo wa miaka 35 na kumuua papo hapo siku ya Jumatatu, Agosti 27 2019 nyakati za usiku.

Kwa mujibu wa Daily Nation, inadaiwa kuwa mwigizaji huyo alikuwa akiendesha gari kutoka Kaloleni kwenye barabara ya Mazeras pale ambapo alimgonga mwanaume huyo ambaye alikuwa akivuka barabara bila kuchukua tahadhari.

Kamishna Okeri alisema mwigizaji huyo aliachiliwa kwa dhamana baada ya kukamatwa ingawaje gari lake bado linazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kaloleni.

Aliongeza kwamba, mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Coast General mjini Mombasa kabla ya kuzikwa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad