Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson akalia kuti kavu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amepuuza wiito wa kujiuzulu, baada ya uamuzi wa mahakama ya juu kwamba hatua yake ya kuahirisha bunge ilikuwa kinyume na sheria. Vikao vya bunge vimeitishwa tena leo siku ya Jumatano.

Uamuzi huo wa mahakama ya juu zaidi nchini Uingereza umeungwa mkono kwa kauli moja na majaji wake wote 11, hali ambayo inazidisha uzito wa uamuzi huo, na matatizo kwa waziri mkuu Boris Johnson.

Rais wa mahakama hiyo, Lady Hale amesema hatua ya serikali ilikuwa na malengo ya kulitatiza bunge kufanya majukumu yake.

”Kwa hiyo mahakama imehitimisha kwamba uamuzi wa kumshauri Malkia kusitisha shughuli za bunge ulikuwa kinyume na sheria, kwa sababu matokeo yake yalilitatiza bunge, au yalilizuia bunge kufanya majukumu yake ya kikatiba, bila sababu yoyote ya msingi.” Amesema rais huyo wa mahakama ya juu ya Uingereza.


Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya uamuzi huo wa mahakama mjini London, Boris Johnson ambaye yuko mjini New York akihudhuria Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, amepuuza miito iliyotolewa na wanasiasa mbali mbali wakimtaka ajiuzulu, akisema kuwa kwa maoni yake, uamuzi wa mahakama ya juu haukuwa sahihi.

Amesema, ”Inabidi niseme kwamba napingana vikali na uamuzi wa majaji. Sidhani kama ni sahihi, lakini bila shaka tutasonga mbele, na vikao vya bunge vitafanyika tena.”

Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle, Katika hukumu yake, mahakama ya juu imesema hivi sasa ni wajibu wa viongozi wa bunge kuamua muda wa kuanza tena vikao vyao, na tayari spika wa baraza la chini John Bercow, amesema milango ya bunge huko Westminster itafunguliwa leo Jumatano.

Großbritannien Debatte zum Brexit im Unterhaus in London | John Bercow, Speaker (picture-alliance/empics/House of Commons)Spika wa bunge la Uingereza John Bercow
Spika huyo amesema uamuzi wa mahakama ya juu ni wa kihistoria, na kwamba raia wanayo haki ya kuona wawakilishi wao wakitimiza majukumu yao ya kikatiba, ya kuishinikiza serikali kuwajibika.


Miongoni mwa wanasiasa waliomtaka waziri mkuu Boris Johnson kujiuzulu ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour, Jeremy Corbyn, ambaye amemtuhumu Johnson kuidharau misingi ya demokrasia na utawala wa sheria.

Waziri kiongozi wa Scotland, sehemu ya Uingereza yenye mamlaka ya ndani Nicola Sturgeon amekwenda mbali, na kusema ikiwa Johnson hatokuwa na ujasiri wa kujiuzulu mwenyewe, basi wabunge waungane na kumtimua madarakani.

Mratibu wa masuala ya Brexit katika bunge la Umoja wa Ulaya Guy Verhofstadt, amesema hatimaye, katika mvurugano wa Brexit, imedhihirika kuwa utawala wa sheria nchini Uingereza bado uko hai na wenye nguvu.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad