Kocha Yanga Mziki wa Pyramids Hatuwawezi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo amefunguka kuwa wapinzani wao Pyramids wako juu kuliko wao ambapo hawezi kulalamika kwa matokeo ambayo waliyapata walipokutana nao katika Kombe la Shirikisho Afrika.



Zahera Jumapili iliyopita alishuhudia kikosi chake kikikubali kipigo cha mabao 2-1, mbele ya Waarabu Pyramids katika mchezo wa kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe hilo la Shirikisho Afrika.


Kwa sasa Yanga wanajiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Pyramids ambayo itapigwa nchini Misri Novemba 3, huku wakihitaji ushindi wa mabao 2-0 kwa ajili ya kusonga mbele.


Zahera ameliambia Championi Jumatano, kuwa hawezi kulalamika kwa ajili ya matokeo ambayo wameyapata kutoka kwa wapinzani wao kutokana na ukweli kuwa wapinzani wao wako juu kuliko wao. “Hii ni kama bahati mbaya ya kupoteza mchezo huu kama ambavyo ilitutokea kule Zambia tulipocheza na Zesco.

Ukiangalia mabao ambayo wameyapata ni kama yale ya mchezo uliyopita na Zesco lakini hatuwezi kulalamika
sana. “Wengi wanalalamika kwa sababu tulibadilisha uwanja lakini niwaambie mabadiliko haya wala hayajatuathiri kwa kitu chochote kile.
 “Ukweli ni kuwa wenzetu wako juu kuliko sisi na hilo liko wazi na hatuwezi kulalamika kwa sababu wametufunga, kitu cha muhimu ni kuangalia mechi ya pili tutafanya nini,” alimaliza Zahera ambaye anatajwa kuwa anaweza kutimuliwa kwenye timu hiyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad