Maaskofu Wapendekeza Wanaume Waliooa Kuwa Mapadre

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MAASKOFU wa Kanisa Katoliki wapendekeza kuwaruhusu baadhi ya wanaume waliooa kufanya kazi za Upadre.

Pendekezo hili limepitishwa kwa kura 128 dhidi ya 41 zilizokataa. Hata hivyo lazima Papa Francis apitishe pendekezo hili na endapo liruhusiwa, basi hii itakuwa ni Historia kubwa ambayo itakuwa imewekwa na Kanisa hilo tangu kuanzishwa kwake.

Ruhusa hii itazihusu nchi za Bolivia, Brazil, Colombia, Ecuador, French Guiana, Guyana, Peru, Suriname, na Venezuela ambazo imethibitika kuwa kuna uhaba mkubwa wa Mpadre.



Kwa sasa kanisa hilo linaruhusu watu wasiooa tu ndiyo hupewa daraja takatifu la Upadre, lakini kwa Waanglikana wapo wanaoruhusiwa kuwa mapadre hata kama wameoa.

Katika mkutano Mkubwa wa Synod uliofanyika kwa wiki tatu na kumalizika Jumamosi iliyopita huko Vatican, ukihusisha maaskofu 184 kutoka sehemu mbalimbali duniani, masista na watumishi wengine wa kanisa hilo, walisema nchi za ukanda wa Amazon ndizo zinaathirika zaidi kwa kukosa mapadre kutokana na kikezo cha kutooa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad