Mimba 229 za wanafunzi zamkera JPM, awafunda majibu ya kuwapa ‘mafataki’

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekasirishwa na ripoti ya wanafunzi 229 kupewa mimba mkoani Rukwa huku kukiwa na sintofahamu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wanaume waliofanya vitendo hivyo.

Akizungumza katika moja ya mikutano yake ya hadhara mkoani humo, Rais Magufuli ameonesha kushangazwa na idadi hiyo huku akiwanyooshea kidole viongozi wa mkoa huo.

“Kuna tatizo moja nimeliona kwenye mikoa hii ya Rukwa, mimba zimeongezeka. Mwaka 2018 watoto 229 wamepata mimba na sijasikia wanaume 229 wamefungwa zaidi ya miaka 30, na bado wanawatafuta wengine wawape mimba, wakati sheria zipo na Mkuu wa Mkoa yupo,”alisema Rais Magufuli.

“Serikali inatoa mchango kwa kutoa elimu bure na wanaume bure wanawapa mimba watoto wa shule! Hao wanaume bure 229 ndio viongozi? Kwa sababu kama sio hao viongozi, je viongozi wameshindwa kitu gani kuwapeleka hawa watoto kwenye haki?” Rais Magufuli alihoji.

Rais Magufuli aliwasihi viongozi wa dini kuingilia kati na kukemea vitendo hivyo, huku akiwaagiza viongozi wa Serikali kuhakikisha kuwa wanawalinda watoto wa kike dhidi ya ‘mafataki’. Alisema kama kuna mwanafunzi ana mimba kwenye eneo la kiongozi husika basi atambue kuwa hatoshi.

Aliwafunda pia wasichana katika mkoa huo wawape majibu magumu wanaume wanaotaka kuwadanganya ili wawape mimba.

“Ukiambiwa wewe mzuri mwambie akamwambie mama yake, msiogope kuwapa maneno magumu, nataka msome, nyinyi ndio marais wa kesho, mawaziri na wabunge. Hata kama mwalimu wako anakwambia anakupenda penda mwambie hayohayo majibu, takwimu za mimba mkoa huu zinatisha,”alisema Rais Magufuli.

Alisisitiza kuwa takwimu hizo ni aibu kwa mkoa wa Rukwa na zinakinzana na lengo la Serikali kutoa elimu bure hadi Sekondari ili kuwapa nafasi wasichana na wavulana kusoma na kujikomboa kimaisha.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kitengo cha sayansi ya jamii na maendeleo ya jamii hilo wanaliweza na ni jepesi sana kwa kupitia taaluma yao. Mkuu wa mkoa hilo... Hajaspecilize.. Na mahakama.. Itatoa adhabu tu lalini si kumaliza tatizo. Wenye taaluma hizo wamejifunza kuuchimbua mziizi wa tatizo na kutoa dawa muafaka. Kweli inauma sana kwa watoto wetu hao wote kulaghaiwa na wahusika kutowajibishwa. Wakuu wa dini pia sawa kuingilia Kati. Ila tatizo hilo linalo dawa yake likichimbuliwa mziizi wake. Tafiti ni muhimu.

    ReplyDelete

Top Post Ad