Naibu Waziri Mabula ataka vijana kujifunza maisha ya Nyerere kwa vitendo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula amewataka vijana kujifunza maisha ya baba wa Taifa Mwalimu Julius kwa vitendo ili matendo ya kiongozi huyo wa kwanza wa Tanzania yaendelee kukumbukwa.

Akiwa katika Maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya Mwl.  Nyerere katika kanisa Katoliki la Bikira Maria jimbo la Musoma Parokia ya Butiama mkoani Mara jana Dkt Mabula alisema, ni vyema vijana wa watanzania wakatumia hazina ya wazee kama Mwl Nyerere Julius Nyerere kuwa chachu ya kuishi kwa vitendo.

"Niwaombe vijana kutumia hazina ya wazee wetu na kuwa chachu ya kuishi kwa vitendo" alisema Dkt Mabula.

Dkt Mabula ambaye alikuwa Mkuu wa kwanza wa wilaya ya Butiama mkoani Mara  alihitimisha salamu zake za miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere wilayani Butiama kwa kuwataka wananchi kuishi pia kwa kumcha Mungu kwa kuwa wakati wa uhai wake baba wa taifa aliishi kwa kumcha Mungu.


Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba alimueleza Mwl Nyerere kuwa alikuwa ni mtu wa maisha ya Mungu aliyejitahidi kujenga umoja na mshikamano kwa nchi yake na Bara la Afrika kwa ujumla.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Phillip Mangula alimuelezea Mwl Nyerere kama mtu aliyepigania haki na aliyesisitiza kuwa binadamu wote ni ndugu na Afrika ni moja
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad