Rais Magufuli Amfuta Kazi Kamanda wa TAKUKURU Mtwara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo Jumatano, Oktoba 16, 2019 amemfukuza kazi Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara, Stephen Mafipa baada ya kumuita mkutanoni wilayani Masasi akawa hayupo.



Magufuli alimuita Kamanda huyo kutokana na malalamiko ya wananchi wa eneo hilo wakidai kudhulumiwa pesa zao za korosho mwaka juzi 2017, huku waliotafuna pesa hizo wakitoroka na kutokomea kusikojulikana.



Magufuli amempigia simu Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo na kumuagiza kuteua Kamanda mwingine leo wa TAKUKURU mkoani humo.



“Brigedia Jenerali, nipo hapa Masasai, nimemuita Kamanda wako wa TAKUKURU hapa hayupo, nimemfuta kazi hapahapa. Sasa nakuagiza leo hii uteue Kamanda mwingine, aje hapa asaidizane na RPC kuwakamata hao wezi na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria.



“Hatuwezi tukavumilia huu ujinga na siwezi kukubali wananchi wangu wakanyanyasika. nataka utekeleze mara moja,” amesema Magufuli wakati akitoa maelekezo hayo kwa Brigedia Jen. Mbungo kupitia njia ya simu ya mkononi.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad