Anayedaiwa Kumuua Naomy, Kesi Yafikia Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


MAPEMA leo Jumatatu, Novemba 4, 2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili Mfanyabiashara Hamis Said (38) umedai kuwa jarada bado lipo kwenye hatua ya mwisho ya uchapaji.

Hayo yamesemwa na wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Salum Ally kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umekamilika.

Wakili Wankyo amedai kuwa jarada lipo kwenye hatua ya uchapishaji hivyo anaiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza shauri hilo, Salum Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 18, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.



Mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad