11/13/2019

Ebitoke: Simtaki tena Mlela, fujo zangu zote kuna kitu nataka alete


Msanii wa vichekesho aliyepata umaarufu kupitia mtandao wa Instagram Anastazia Exavery maarufu kama Ebitoke jana alitamba kwenye kurasa mbalimbali za mtandao ya kijamii pamoja na kurasa mbalimbali za blogu hapa nchini walipoandika kufuatia tukio la kihistoria ambalo wanadada huyo alilifanya la kuvamia mkutano wa Yusuph Mlela ambaye anadaiwa kuwa aliwahi kutokana nae kimapenzi.

Ambapo Ebitoke alivamia na kufanya fujo kadhaa ikiwa pamoja na kumvamia mwanamke mpya anayedaiwa kuwa kwa sasa ndiye mpenzi mpya wa Yusuph Mlela.

Leo Dar24 Media imegonga hodi nyumbani kwa Ebitoka na kufanya nae ”Exclusive” mara baada ya kupiga naye stori kuhusu tukio hilo na mahusiano yake na msanii huyo.

Ambapo Ebitoke amesema kuwa tayari ameachana na Yusuph Mlela ila amefanya fujo hizo akidai kuwa kuna kitu chake kipo kwa Mlela ambapo akishakipata atacha kumsumbua.

”Nilikubali, ukikubali hauwezi ukapata shida, mi nilishakubali kuachana nae, lakini kuna kitu anakijua nataka ndio maaana nafanya hizi fujo, wala ata mi nishaachana nae sina shida nae, fujo zangu zote kuna kitu nataka alete, tuwe sawa tuwe na waashikaji kabisaa” amesema Ebitoke.

Pia ameongezea kuwa ana mambo mengi ambayo anayajua kuhusu Mlela na amesema kuwa akiamua kumchafua naweza kumchafua dunia nzima, ila hana haja ya kufanya hivyo zaidi ya kumtaka ampe hiko kitu chake ambacho anakihitaji kutoak kwake.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Weka Comment Yako Hapa Chini:
Share:
Loading...

0 [disqus]:

Post a comment

Click Below to Subscribe

Popular Posts

Loading...

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger