Kocha Mzawa Akabidhiwa Simba Dar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


UONGOZI wa Simba chini ya mtendaji mkuu, Senzo Mazingisa raia wa Afrika Kusini umemkazia kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems kwa kumsimamisha kazi hadi watakapomjadili huku majukumu yake akipewa kocha mwingine.



Aussems amesimamishwa kuisimamia timu hiyo aliyoipa mafanikio msimu uliopita baada ya kuifikisha robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kuondoka nchini kimyakimya bila ya kutoa taarifa kwa waajiri wake kwa muda wa siku tatu hali iliopelekea kukumbana na panga hilo.



Katika mazoezi yaliyofanyika jana Jumanne kwenye Uwanja wa Gymkhana, Simba ilikuwa chini ya kocha msaidizi, Denis Kitambi mwenye leseni B ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) akisimamia mazoezi hayo kwa muda wa saa tatu kutoka saa tatu asubuhi hadi saa tano na dakika 30. Kitambi ni miongoni mwa makocha wachache wazawa wenye sifa za kimataifa.



Championi Jumatano, ambalo lilikuwepo uwanjani hapo lilimshuhudia Kitambi, akisaidiwa na kocha wa viungo, Adel Zrane na kocha wa makipa Mohammed Mwarami ambapo alianza kwa kuwakimbiza wachezaji kwelikweli.



Kitambi aliwagawa wachezaji kwa makundi matatu ambao walikimbia katikati ya uwanja kwa spidi kubwa na ndogo kwa muda wa dakika 30 kabla ya kuwabadilishia mazoezi mengine ambayo yalitumia muda mwingi umilikiji wa mpira.



Lakini Kitambi ambaye alikuwa akisaidiwa na wasaidizi wake alitumia muda mwingi katika zoezi la kufunga mabao kwa kuwatumia, Meddie Kagere na Miraj Athuman ‘Sheva’ ambao walikuwa wakifunga kwa mpira ya krosi iliyokuwa ikipigwa na mawinga wa pembeni huku katika zoezi hilo kiungo Clatous Chama akifunga mabao matano wakati Kagere na Sheva wakifunga mabao mawili kila mmoja.



Akizungumza na Championi Jumatano, Kitambi alisema kuwa kwa sasa amekabidhiwa majukumu ya kuifundisha timu hiyo na mtendaji mkuu kwa muda wa wiki moja wakati wakisubiria mustakabali wa kocha mkuu Patrick Aussems aliyesimamishwa.



“Nimekabidhiwa kusimamia majukumu na programu zote za timu na mtendaji mkuu kwa sababu mwalimu yeye amesimamishwa hadi pale watakapokaa chini na uongozi kumjadili.



“Hili ni jukumu la wiki moja kwa maelezo niliyopewa kwa kuwa mwalimu anakutana na uongozi kesho (leo) ili kujua kama ataendelea kuwepo au nini kitatokea, kikubwa mashabiki wawe watulivu wakati uongozi unajaribu kuweka mambo sawa,” alisema Kitambi.



Kitambi aliongeza kuwa: “Lakini kwa upande wa wachezaji hawapo sawa kisaikolojia kutokana na hali inayoendelea sasa ingawa naamini ni kitu cha kawaida na watakaa sawa.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad