Lori la Mafuta Laua Watatu DSM, Dereva akimbia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jumla ya watu watatu wamefariki Dunia papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya, baada ya kugongwa na Lori la mafuta lililoacha njia na kuparamia watembea kwa miguu, maeneo ya Mlimani City, lililokuwa likitokea Ubungo kwenda Mwenge.


Gari lenye namba za usajili T828 BCD, Tela namba T419 AUD, lililopata ajali maeneo ya Mlimani City.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, leo Novemba 23, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu, amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 5:20 asubuhi, ambapo mara baada ya ajali hiyo kutokea, dereva alikimbia na kutoweka kusikojulikana.

"Dereva aliacha njia na kugonga watembea kwa miguu, kati ya watu wanne waliogongwa watatu walifariki papo hapo na mmoja ni majeruhi amepelekwa hospitali, mmoja aliyefariki ametambulika kwa jina la Daniel Mushi ni fundi umeme na mkazi wa Kimara - Temboni, ni uzembe tu wa dereva maana aliacha njia na kuparamia watembea kwa miguu" amesema Kamanda Taibu.

Kwa mujibu wa Kamanda Taibu, miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali hiyo na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kufanya juhudi za kumsaka dereva huyo popote alipo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad